DK MOLLEL AWASHUKIA WATUMISHI WA UMMA WANAOFUNGIA VITUO VYA KULELEA WATOTO
Muhtasari: Maofisa ustawi wa jamii wametakiwa kuacha tabia ya kuvifungia vituo vya kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na hatarishi bila kuwa na mbadala wa mahali pa kuwapeleka watoto hao. Na Mwandishi Wetu, Dodoma. NAIBU Waziri wa afya, Dk Godwin Mollel amewataka watumishi wa umma kuacha kuvifungia vituo vya kulelea watoto bila kujua watawapeleka wapi watoto hao baada ya vituo hivyo kufungwa. Dk Mollel ametoa kauli hiyo leo alhamisi Juni 27, 2024 wakati akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa kituo cha kulelea watoto wanaloishi kwenye mazingira magumu na hatarishi Kisedet kilichopo Kata ya Chigongwe Jijini Dodoma. Dk Mollel amesema kitendo hicho kinawakatisha tamaa watu ambao wamejitolea kuwalea watoto katika mazingira waliyonayo hivyo badala ya kuvifungia vituo hivyo wanatakiwa waviboreshe ili watoto wasizagae hovyo mitaani. "Unakuta mtu ameamua kuwakusanya na kuwalea watoto baada ya kuwaokota huko mitaani anakuja mtumishi wa umma anakifunga hicho kituo...