MWANDISHI WA HABARI MATHIAS CANAL ACHANGIA SH MIL 1 KWA AJILI YA MADAWATI

 Mutasari: Shule ya msingi  Kigasha  imejengwa kwa nguvu ya wananchi wa jimbo hilo ambao wamejenga madarasa mawili na Mbunge wake Innocent Bashungwa alichangia mabati kwa ajili ya kupaua

Na Mwandishi Wetu, Karagwe

KUFUATIA juhudi zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo la Karagwe Innocent Bashungwa katika kuimarisha sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Kigasha, Mwandishi wa habari nchini  Mathias Canal amechangia kiasi cha Shilingi Milioni 1 kwa ajili ya madawati.

Mathias amechangia madawati hayo mara baada ya kutembelea shule hiyo iliyopo katika kata ya Rugu, Tarafa ya Nyaishozi Wilayani karagwe Mkoani Kagera akiwa katika kazi ya kutembelea miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya kujionea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/2025.




                                                     Mwandishi wa habari nchini Mathias Canal

Canal amesema kuwa usimamizi wa ujenzi wa shule hiyo unaenda sambamba na serikali kupeleka walimu ambapo ametumia nafasi hiyo kumpongeza Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda kwa kuweka kipaumbele katika shule hiyo ili kuhakikisha wanafunzi wa maeneo hayo wanapata elimu bora kama ilivyo katika maeneo mengine nchini.

Kwa upande wake katibu wa Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Ivo Ndisanye amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa shule na upatikanaji wa walimu.

Pia kwa niaba ya Mbunge wa jimbo hilo Innocent Bashungwa katibu huyo ameahidi kuchangia Mil 3 kwa ajili ya upatikanaji wa madawati ili kuimarisha ufanisi wa kujifunza.



Ivo amewapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi katika kijiji hicho kwani kupitia nguvu za wanachi wameweza kujenga madarasa mawili ambayo mbunge alitoa mabati kwa ajili ya kupaua.



Comments

Popular posts from this blog

CHODAWU YAITAKA SERIKALI KURIDHIA MKATABA NAMBA 189 WA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI

NGOs ZAPEWA MWONGOZO WA KULIPA KODI NA TRA

TMDA YATOA MSAADA WA DAWA NA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SH 24 MILIONI