ESWATIN YAJA KUJIFUNZA NAMNA YA KUENDESHA MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII PSSSF
Muhtasari: Ujumbe wa watu tisa kutoka nchini Eswatin wametembelea mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSSSF ili kujifunza namna bora ya uendeshaji wa mifuko ya pensheni na kuachana na mfuko wa akiba ambao bado unatumika nchini humo. Na Mwandishi Wetu, Dodoma SERIKALI imesema kuwa itapeleka wataalam wa kuendesha mifuko ya hifadhi za jamii kutoka mfuko wa PSSSF nchini Eswatin ili kuwafundisha namna kuanzisha mfuko wa hifadhi ya jamii unaotoa pensheni kwa wanachama wake na kuachana na mfuko wa akiba ambao unatumika nchini humo kwa sasa. Hayo yamesema leo ijumaa Julai 19, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSSSF Abdul-Razaq Badru baada ya kupokea ujumbe wa viongozi tisa akiwemo waziri wa utumishi wa umma kutoka nchini Eswatin kwa ajili ya ziara ya kuja kujifunza uendeshaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii inayotoa pensheni kwa wanachama wake. Badru amesema nchi ya Eswatin bado inatumia mfuko wa akiba kwa wanachama wake na wanataka kuanza kutoa pensheni hivyo wamekuja kujifunza n...