Posts

Showing posts from September, 2024

POLISI DODOMA KUKABILIANA NA VITENDO VYA UHALIFU

Image
Muhtasari: Kutokana na kushamiri kwa matukio ya ukatili Mkoani Dodoma dawati la jinsia na watoto la polisi limekuja na kampeni kabambe ya kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto mkoani humo. Na Mwandishi Wetu, Dodoma  DAWATI la jinsia na watoto la polisi mkoa wa Dodoma limekutana kwenye kikao kazi maalum cha kujadili matukio ya ukatili yanayoendelea mkoani humo ili kujua namna ya kukabiliana nayo. Mkuu wa dawati la jinsia Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni  mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi Christer Kayombo ameyasema hayo leo alhamisi Septemba 17, 2024  kwenye kikao kazi kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa kupinga ukatili wa kijinsia na watoto Jijini Dodoma. Christer amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kwa polisi wa dawati la jinsia na watoto  kwa lengo la kuwawezesha kuondoa matukio ya ukatili ambayo yameshamiri katika mkoa wa Dodoma. “Sisi kama mkoa tuliona ipo haja ya kufanya kitu cha ziada ili kupambana na matendo ya ukatili, tukaamua kuandaa mafunzo h...

KUFUNGULIWA KWA MASOKO YA MAZAO NJE YA NCHI FURSA KWA WAKULIMA NCHINI

Image
 Muhtasari: Serikali ya Tanzania kuingiza kiasi cha fedha dola za Marekani 3.5 bilioni kwa mwaka kutokana na mauzo ya mazao nje ya nchi. Na Mwandishi Wetu, Dodoma  SERIKALI imesema itaingiza kiasi cha fedha dola za marekani 3.5 bilioni kwa mwaka kwa kuuza mazao ya kimkakati  nje ya nchi kwa mwaka. Hayo yameelezwa leo Alhamisi Septemba 19, 2024 na Naibu waziri wa kilimo David Silinde kwenye hafla ya uzinduzi wa mchakato wa kufungua masoko mapya ya mazao ya kipaumbele Jijini Dodoma. Silinde amesema hivi sasa nchi imepata kibali cha kuuza mazao tisa ya kiupaumbele kwenye nchi 14 ambayo yataliingizia taifa kiasi cha fedha Dola za Marekani 3.5 bilioni na kuwataka wakulima nchini kuchangamkia fursa hiyo. Ameyataja mazao hayo ya kipaumbele kuwa ni nanasi, ndizi, tumbaku, parachichi, viazi mviringo, karafuu, pilipili manga, vanilla, na kakao ambayo yatauzwa kwenye nchi 14 duniani. “Nchi hizo ni pamoja na China ambao wanahitaji vanila na nanasi, India (vanilla na nanasi), Indonesi...

TAASISI ZA BIMA ZITOE ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU UMUHIMU WA KUKATA BIMA

Image
  Muhtasari: Taasisi za Bima nchini zimeshauriwa kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kukata bima kwenye shughuli wanazofanya   kwa wananchi ambao inadaiwa wengi wao hawana uelewa wa huduma zinazotolewa na taasisi hizo. Na Mwandishi Wetu, Dodoma MAMLAKA ya usimamizi wa bima nchini (TIRA) kwa kushirikiana na wadau wa bima wameshauriwa kutoa elimu ya bima kwa wananchi hasa yanapotokea majanga kwa wateja wao ili wananchi wengi wajue umuhimu wa kukatia bima shughuli zao za uchumi. Ushauri huo umetolewa leo ijumaa, Septemba 13, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, kwenye matembezi ya kuadhimisha siku ya bima nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Mayanja amesema ni Watanzania wachache wenye uelewa kuhusu huduma za bima na kundi kubwa halina elimu hivyo yanapotokea majanga kwa wateja wao wenye bima basi watumie fursa hiyo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuwa na bima. Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma, Janeth Mayanja “Nina fahamu Tir...

BONDE LA CONGO NA AJENDA YA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Image
Muhtasari: Tanzania, Kamisheni ya Tabianchi ya Bonde la Congo na Mfuko wa Bluu wa Bonde la Congo Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Na Mwandishi Wetu, Dodoma KATIKA juhudi za kuboresha uhifadhi wa mazingira nchini, Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imefanya mkutano na Kamisheni ya Tabianchi ya Bonde la Congo (CBCC) pamoja na Mfuko wa Bluu wa Bonde la Congo (CBFF) jijini Dodoma.  Mkutano huo umejikita katika kuimarisha mikakati ya pamoja ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kuongeza ushirikiano kati ya pande hizi tatu katika juhudi za kulinda mazingira na kuendeleza uhifadhi. Akiongea na waandishi wa habari leo Jumatano Septemba 11, 2024 mara baada ya kumalizika kwa kikao cha ndani, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk. Pindi Chana amesema mkutano huo unalenga kuimarisha juhudi za kulinda mazingira za kikanda na kukuza suluhu za pamoja kwa mabadiliko ya hali ya hewa na uhifadhi wa utofauti wa kibaiolojia kat...

THB YALAANI MAUAJI YANAYOENDELEA NCHINI

 Muhtasari: Tume ya haki za binadamu na utawala Bora nchini (THBUB) imelaani mauaji ya watu yanayoendelea nchini na kuwatwisha jukumu la kukomesha mauaji hayo jeshi la polisi, viongozi wa serikali za mitaa, viongozi wa dini asasi za kiraia, vyombo vya habari na wananchi wenyewe. Na Mwandishi Wetu, Dodoma  Dodoma. Mwenyekiti wa Tume ya haki za binadamu na utawala Bora nchini (THBUB) Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema tume hiyo inalaani mauaji ya watu yanayoendelea nchini na kuitaka jamii kuishi kwa kufuata sheria na kuheshimu haki ya msingi ya kila mtu kuishi. Jaji Mwaimu ametoa kauli hiyo leo Ijumaa, Agosti 30, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matukio ya mauaji kwa watu ya ayoendelea nchini Jijini Dodoma. Jaji Mwaimu amesema kuwa hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la mauaji ya kutisha ambayo yanaendelea nchini ambayo yameripotiwa na vyombo vya habari na jeshi la polisi na kwamba tume hiyo inalaani matukio hayo na kuzitaka mamlaka zinazohusika kuchukua hatu...