THB YALAANI MAUAJI YANAYOENDELEA NCHINI

 Muhtasari: Tume ya haki za binadamu na utawala Bora nchini (THBUB) imelaani mauaji ya watu yanayoendelea nchini na kuwatwisha jukumu la kukomesha mauaji hayo jeshi la polisi, viongozi wa serikali za mitaa, viongozi wa dini asasi za kiraia, vyombo vya habari na wananchi wenyewe.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

Dodoma. Mwenyekiti wa Tume ya haki za binadamu na utawala Bora nchini (THBUB) Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema tume hiyo inalaani mauaji ya watu yanayoendelea nchini na kuitaka jamii kuishi kwa kufuata sheria na kuheshimu haki ya msingi ya kila mtu kuishi.

Jaji Mwaimu ametoa kauli hiyo leo Ijumaa, Agosti 30, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matukio ya mauaji kwa watu ya ayoendelea nchini Jijini Dodoma.

Jaji Mwaimu amesema kuwa hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la mauaji ya kutisha ambayo yanaendelea nchini ambayo yameripotiwa na vyombo vya habari na jeshi la polisi na kwamba tume hiyo inalaani matukio hayo na kuzitaka mamlaka zinazohusika kuchukua hatua ili kukomesha matukio hayo.

Amesema tume hiyo inalaani wimbi la mauaji ya ayoendelea hapa nchini kutokana na baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi na kusababisha mauaji ya kikatili katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema matukio hayo yamekuwa yaliripotiwa na vyanzo mbalimbali vya taarifa hususani vyombo vya habari na taarifa zinazotoka kwenye jeshi la polisi nchini.

"Pamoja na serikali na wadau kulaani vitendo hivyo mauaji hayo yameendelea kushika kasi licha ya jeshi la polisi kufanya jitihada za kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria," amesema Jaji Mwaimu.

Mwenyekiti huyo amesema baada ya kufuatilia mauaji hayo tume imebaini kujengewa tabia za baadhi ya wananchi kutozingatia sheria za nchi na kujichukulia sheria mkononi na kwamba vitendo vya mauaji vilivyotokea mfululizo hivi karibuni vimetokana na ukatili dhidi ya binadamu.

"Katika baadhi ya mauaji yaliyotokea kuna viashiria vya ulipaji kisasi, wivu wa kimapenzi, imani za kishirikina na baadhi ya wananchi wanajenga dhamankuwa wanaweza kutenda uovu na wasiweze kukamatwa na wananchi hawana Imani na vyombo vya usimamizi wa sheria na haki na uwepo wa wananchi wasiopenda kufanya kazi halali na hivyo kuwa na tamaa ya mali," amesema Jaji Mwaimu.

Amesema kutokana na mauaji hayo ya kikatili Tume inatamka kwamba vitendo vya mauaji yaliyotokea hivi karibuni ni ukiukwaji wa haki ya kuishi kama ilivyotamkwa kwenye ibara ya 14 ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na hivyo inalaani vikali vitendo hivyo.

Amesema ili kukomesha mauaji hayo tume inapendekeza jeshi la polisi liendelee kuchukua hatua mahsusi kuimarisha mifumo ya ulinzi kwenye maeneo ya wananchi ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa za mapema kuhusu kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa sheria vinavyopelekea kuwepo mauaji na vitendo vya ukatili kabla matukio hayo kutokea kwa kushirikiana na wananchi  katika maeneo husika ili kusaidia ulinzi na usalama wa raia.

"Pia jeshi la polisi liendelee kuchukua hatua ili kuhakikisha watu wote wanaohusika na mauaji hayo wanakamatwa ili sheria ichukue mkondo wake na mamlaka za serikali za mitaa tume inapendekeza mamlaka hizo katika ngazi zote ziwe na Mipango madhubuti za kuhakikisha zinakiwepo taratibu za kuimarisha ulinzi na usalama wa raia kwa kushirikiana na jeshi la polisi katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za mapema katika kushughulikia matukio ya uhalifu kwa kushirikiana na mamlaka husika kuhusu masuala ya kijamii yanayojitokeza kwenye mitaa yao," amesema.

Kuhusu viongozi wa dini tume imewataka kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu ya dini za maadili na kukemea uovu unaotokea nchini na kuwataka wananchi kujengabutamaduni wa kuheshimu sheria za nchi na haki za binadamu kwa wengine kwa kutambia kwamba namna bora ya kupata suluhu ya migogoro inayowakabili katika ngazi zote za jamii ni kushughulikia migogoro hiyo kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa badala ya kujichukulia sheria mkononi.

Amewataka wananchi washirikishe vyombo vya Dola wanapoona maovu yakitendeka ndani ya jamii na kufichua uvunjifu wowote wa sheria na haki za binadamu na kusaidia katika upelelezi wa matukio hayo na wananchi waishio vijijini waendelee utamaduni wa kujuliana hali wanapoamkw asubuhi na linapotokea jambo linaloashiria uvunjifu wa amani ndani ya familia washirikishe vyombo vya Dola ili wazuie madhara ya ayoweza kutokea ikiwemo mauaji.


Amewataka wananchi wakumbuke kulinda utu wa binadamu kwa gharama yoyote kwa kuwa haki ya kuishi ni haki ya msingi kwa kila mtu.

Aidha tume imependkeza asasi za kiraia na vyombo vya habari waendelee kutoa elimu kwa umma kuhusu taratibu zilizopo za namna ya kughulikia masuala mbalimbali ya kijamii pitia sheria na hivyo kulinda haki za binadamu na utu wa mtu.

Mwisho......

Comments

Popular posts from this blog

CHODAWU YAITAKA SERIKALI KURIDHIA MKATABA NAMBA 189 WA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI

NGOs ZAPEWA MWONGOZO WA KULIPA KODI NA TRA

TMDA YATOA MSAADA WA DAWA NA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SH 24 MILIONI