Posts

Showing posts from August, 2024

TSC YAKABIDHIWA MAGARI KWA AJILI YA KUTEMBELEA WALIMU NA KUJUA CHANGAMOTO ZAO

Image
Muhtasari: Tume ya utumishi wa walimu imetakiwa kutatua changamoto na kero za walimu nchini na kama kuna wenye changamoto za kisaikolojia watafutiwe huduma ya ushauri nasaha ili wawasaidie utekeleza majukumu yao ya kutoa elimu wa Watanzania. Na Mwandishi Wetu, Dodoma WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ameiagiza tume ya utumishi wa walimu (TSC) kughulikia kero na changamoto za walimu nchini ili kuondoa malalamiko yote ya walimu na kama kuna walimu watakuwa na changamoto za kisaikolojia wawape huduma ya ushauri nasaha. Mchengerwa ameyasema hayo leo jumapili Agosti 11, 2024  wakati akikabidhi magari 10 kwa makatibu wasaidizi wa wilaya wa tume ya utumishi wa walimu jijini Dodoma na kuwataka kuyatumia magari hayo kuwatembelea walimu kwenye vituo vyao vya kazi ili kujua changamoto walizonazo badala ya kukaa maofisini na kusubiri walimu wawafuate. Sehemu ya magari 10 ambayo yamewagawiwa kwa makatibu wasaidizi wa Wilaya wa tume ...

BILA TASAF NISINGEFIKA CHUO KIKUU KUSOMEA UHANDISI AMBAYO NI NDOTO YANGU

Image
Muhtasari: Mwanafunzi wa uhandisi wa Mawasiliano kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Habiba Maramoja ameelezea namna Mpango wa kunusuru kaya maskini (Tasaf) ulivyomsaidia kutimiza ndoto zake kwani bila wao asingeweza kusoma chuo kikuu. Na Mwandishi Wetu, Dodoma MWANAFUNZI wa mwaka wa tatu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), anayesomea uhandisi wa mawasilino, Habiba Maramoja amesema kama familia yao isingeingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini (Tasaf) asingeweza kufikia ndoto zake za kusomea kozi hiyo kutokana na umaskini waliokuwa nao kabla ya kuingizwa kwenye mpango. Akizungumza leo Alhamis, Agosti 8, 2024 kwenye maonyesho ya wakulima nanenane Jijini Dodoma, Habiba amesema familia yao ni miongoni mwa kaya maskini zilizosaidiwa na Tasaf kwani walikuwa hawawezi kupata milo mitatu kwa siku kwa kuwa walikuwa wanaishia mlo mmoja kwa siku na wakati mwingine walikuwa hawapati kabisa. Amesema kaya yao iliingia kwenye mpango wa Tasaf mwaka 2014 na wakati huo alikuwa kida...

NEMC YAJA NA MRADI WA MAJOSHO KUTUNZA VYANZO VYA MAJI

Image
 Muhtasari: Ili kutunza na kulinda mazingira kwenye vyanzo vya maji, Baraza la Taifa la  Usimamizi wa mazingira (NEMC) limeanzisha miradi ya majosho kwa wafugaji ili kuzuia wanyama kubomoa kingo za mito pale wanapokwenda kunywa maji. Na Mwandishi Wetu, Dodoma  BARAZA la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeanzisha mradi wa majosho kwa wafugaji wanaoishi kwenye vyanzo vya maji na kando ya mito ili kutunza vyanzo hivyo visiharubiwe na wanyama pale  wanapokwenda kunywa maji. Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Mazingira Mkuu kutoka NEMC, Innocent Makomba wakati akizungumza kwenye maonyesho ya wakulima nanenane kuhusu hatua zinazochukuliwa na baraza hilo kulinda vyanzo vya maji nchini Jijini Dodoma. Ofisa Mazingira mkuu kutoka NEMC Innocent Makomba akizungumza kuhusu uanzishwaji wa majosho kwenye maeneo ya wafugaji ili kulinda vyanzo vya maji nchini kwenye maonyesho ya wakulima nanenane Jijini Dodoma leo Agosti 6, 2024 Makomba amesema kunywesha maji kwenye vyanzo vya ma...

NIC IMEWATAKA WAKULIMA KUKATA BIMA YA FIDIA ILI KUJILINDA NA MAJANGA YA TABIANCHI

Image
Muhtasari: Shirika la bima la Taifa limewataka wakulima kukatia bima ya fidia mazao yao ili kujikinga na majanga ambayo hayazuiliki. Na Mwandishi Wetu, Dodoma  SHIRIKA la bima la Taifa limewataka wakulima wafugaji na wavuvi kukatia bima ya fidia mazao yao ili kujikinga na majanga ambayo hayazuiliki. Wito huo imetolewa leo Ijumaa Agosti 2, 2024 na Ofisa maendeleo mwandamizi kutoka Shirika la bima la Taifa (NIC), Nicholaus Malakasuka wakati akizungumza kwenye maonyesho ya wakulima nanenane Jijini Dodoma. Ofisa maendeleo mwandamizi kutoka Shirika la bima la Taifa (NIC), Nicholaus Malakasuka akizungumza kwenye maonyesho ya wakulima nanenane Jijini Dodoma Leo Agosti 2, 2024 Malakasuka amewataka wakulima, wafugaji na wavuvi kukatia bima ya fidia shughuli wanazofanya ili kujilinda na majanga mbalimbali yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira. Amesema NIC inatoa bima za fidia kwenye shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi ili kuwawezesha wananchi hao kuendelea na sh...

WATAALAMU WAASWA KUPELEKA TEKNOLOJIA YA MIFUGO NA UVUVI VIJIJINI

Image
* Muhtasari: Wataalam waaswa kupeleka teknolojia ya uvuvi vijijini. Na Mwandishi Wetu, Dodoma  MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewaaasa wataalamu wa mifugo na uvuvi kupeleka na kufundisha teknolojia ya mifugo vijijini ili kuwapa wafugaji elimu ya kutosha kuhusu ufugaji wa kisasa kwa lengo la kuleta tija katika sekta hiyo. Akizungumza, leo Agosti 4, 2024 mkoani Dodoma alipotembelea kwenye Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa mkoani Dodoma katika mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Senyamule amesema wataalamu wahakikishe teknolojia hii inawafikia wadau wote wa mifugo na uvuvi, ususani maeneo ya vijijini. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, (wa kwanza kulia), akielezewa na Ofisa maendeleo ya jamii wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Beatrice Mwijage (wa kwanza kushoto), juu ya Mpango wa unywaji Maziwa Shuleni, mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ni  katika Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa Mko...

TEKNOLOJIA YA KISIKI HAI IMEOKOA MITI ZAIDI YA MIL 21 NCHINI

Muhtasari: Kisiki hai chaokoa zaidi ya  miti milioni 21 nchini kwenye Mikoa ya Singida, Dodoma, Manyara, na Arusha  Rachel Chibwete, Dodoma TEKNOLOJIA ya kisiki hai imeokoa zaidi ya miti milioni 21 nchini kwenye Mikoa ambayo haina mvua za kutosha kuotesha miti mipya na hivyo kusaidia kurejesha uoto wa asili kwenye Mikoa hiyo. Akizungumza kwenye maonyesho ya nanenane Mkoani Dodoma, Ofisa kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Lead Foundation, Hagali Mbulla amesema programu ya kisiki hai imesaidia kurejesha uoto wa asili kwenye Mikoa ya Singida, Dodoma, Manyara na Arusha. Amesema Mikoa hiyo minne haina mvua za kutosha kuotesha miti mipya na kuimwagilia kwani miti mingi inayopandwa  hukauka kwa kukosa maji wakati wa kiangazi. "Ili kurejesha uoto wa asili tumewaelekeza wakulima kupogolea miti ya asili iliyopo kwenye mashamba yao itakayowezesha miti hiyo kuendelea kukua badala ya kupanda miti mipya ambayo huwa inakauka kwa kukosa maji kwa sababu hii mikoa hupata mvua chache...

ASA YAJA NA MBEGU YA NGANO INAYOSTAWI MKOA WA DODOMA

Image
 Muhtasari: Wadau wa sekta ya kilimo wamekuja na teknolojia mbalimbali za kilimo za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuwawezesha wakulima kulima kisasa na kupata mazao bora. Rachel Chibwete, Dodoma WADAU wa kilimo wamekuja na teknolojia mbalimbali za kilimo ambazo zitawasaidia wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kujiepusha na uharibifu wa mazingira. Hayo yamebainika leo  jumapili Agosti 4, 2024 kwenye maonyesho ya kilimo nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma. Akizungumza kwenye maonyesho hayo, Ofisa kilimo kutoka wakala wa mbegu nchini (ASA), Benjamin Mfupe amesema wamekuja na mbegu za ngano ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa kwenye ardhi ya Dodoma ambayo haina historia ya kulima zao hilo. Ofisa kilimo kutoka wakala wa mbegu nchini (ASA) Benjamin Mfupe akionyesha zao la alzeti kwenye kitalu kilichopo kwenye viwanja vya maonyesho ya wakulima nanenane Jijini Dodoma  Amesema wamepanda ngano kwa majaribio  kw...

IDADI YA MIFUGO NCHINI IMEONGEZEKA NA KUFIKIA MIL181.9

Image
 Muhtasari: Serikali imetaja ongezeko la idadi ya wanyama wa kufugwa nchini ambayo kwa mwaka 2023/24 imeongezeka na kufikia milioni 181.9 kutoka mifugo 173.1 mwaka 2022/23. Na Mwandishi Wetu, Dodoma NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti amesema idadi ya mifugo nchini imeongezeka kutokana na usimamizi mzuri unaofanywa na sekta ya mifugo na uzalishaji wa mazao ya mifugo kwa kutumia teknolojia za kisasa. Mnyeti ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Agosti 2, 2024 kwenye maonyesho ya wakulima nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma. Amesema hadi kufikia mwaka 2023/2024 Tanzania ilikuwa na jumla ya ng’ombe milioni 37.9, mbuzi milioni 27.6, kondoo milioni 9.4, nguruwe milioni 3.9 na kuku milioni 103.1 ambapo kuku wa asili ni milioni 47.4 na kuku wa kisasa milioni 55.7.  Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Alexander Mnyeti akizungumza kwenye maonyesho ya wakulima nanenane Jijini Dodoma  Naibu waziri huyo amesema ongezeko hilo ni tofauti na ilivyokuw...

WMA YATOA ELIMU KUHUSU MATUMIZI YA VIPIMO SAHIHI KWA WAKULIMA

Image
 Muhtasari: Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) watoa elimu kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya vipimo kwenye biashara ya mazao na kuachana na vipimo vya magunia, visado, madebe, makopo na lumbesa ambavyo vinawapa hasara. Rachel Chibwete, Dodoma ILI kuwawezesha wakulima kutumia vipimo sahihi wakati wa kuuza mazao yao na kuachana na vipimo visivyo sahihi kama vile magunia, visado, makopo madebe na lumbesa, wakala wa vipimo Tanzania  (WMA) umetoa elimu kwa wakulima kuachana na vipimo hivyo. Akizungumza na wakulima waliofika kujifunza kuhusu vipimo sahihi, Ofisa Vipimo kutoka WMA, Said Ibrahim amesema ni wakati wa wakulima kuachana na vipimo visivyo sahihi na kuanza kutumia vipimo sahihi kwa ajili ya maendeleo yao. Ofisa Vipimo kutoka WMA, Said Ibrahim akizungumza kwenye maonyesho ya wakulima nanenane Jijini Dodoma   Amesema kuna utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wa kutumia vipimo visivyo sahihi na hivyo kuwapa hasara wakulima kwani gunia moja linafungwa lumbesa na kuweza ...

BOT KUJA NA KAMPENI KABAMBE YA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUJIEPUSHA NA MIKOPO UMIZA

Image
Muhtasari: Benki kuu ya Tanzania (BOT) yaja na mbinu ya kuwaelimisha wakulima jinsi ya kuondokana na mikopo umiza ambayo haina faida kwenye shughuli zao za uzalishaji mali. Rachel Chibwete, Dodoma ILI kuwaepusha wakulima na mikopo umiza benki kuu ya Tanzania (BOT) imekuja na kampeni ya kutoa elimu ya kujiepusha na mikopo hiyo ambayo huwa inawarudisha nyuma wakulima badala ya kuwaletea maendeleo. Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa Agosti 2, 2024 na Ofisa wa idara ya usimamizi wa huduma ndogo za fedha (BOT), Deogratius Mnyamani, wakati akizungumza na Mwananchi Digital kwenye maonyesho ya wakulima nanenane Jijini Dodoma. Ofisa wa idara ya usimamizi wa huduma ndogo za fedha (BOT), Deogratius Mnyamani akizungumza kwenye maonyesho ya wakulima nanenane Jijini Dodoma  Mnyamani amesema wakulima ni waathirika wa mikopo umiza inayotolewa na watu ambao hawana leseni za kutoa huduma za kifedha na hivyo kujikuta fedha zao zote zinachukuliwa na hao watu. “Kuna watu wanatoa mikopo na kutoza riba hadi...

MAJALIWA ATOA MAAGIZO MANNE KWA WIZARA YA KILIMO NA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI ILI KUKUZA SEKTA HIYO

Image
  Muhtasari: Maonyesho ya kilimo, ufugaji na uvuvi nanenane yamezinduliwa leo Jijini Dodoma katika viwanja vya Nzuguni ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa maagizo manne kwa wizara za kilimo, mifugo na uvuvi, benki ya kilimo (TADB) na maofisa ugani kuwafikia wakulima na kuwasaidia kutafuta masoko ya bidhaa zao. Na Mwandishi Wetu, Dodoma Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefungua maonyesho ya kilimo, mifugo na uvuvi maarufu nanenane na kuziagiza Wizara za kilimo, mifugo na uvuvi kuendelea kusimamia uhifadhi na utunzaji wa mazingira ambayo yatawawezesha kufanya shughuli za kilimo, mifugo pamoja na uvuvi katika eneo la uwanja huo kwa kipindi kirefu. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo alhamisi Agosti 1, 2024 wakati akifungua maonyesho ya kilimo, mifugo na uvuvi kwenye uwanja wa nanenane yanayofanyika kitaifa Nzuguni Jijini Dodoma. Amesema wakiharibu mazingira kwenye maeneo hayo hawatalima kwa sababu hawatapata maji ya umwagiliaji, mito na maziwa itakauka na kuagiza suala...