WATAALAMU WAASWA KUPELEKA TEKNOLOJIA YA MIFUGO NA UVUVI VIJIJINI

*

Muhtasari: Wataalam waaswa kupeleka teknolojia ya uvuvi vijijini.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewaaasa wataalamu wa mifugo na uvuvi kupeleka na kufundisha teknolojia ya mifugo vijijini ili kuwapa wafugaji elimu ya kutosha kuhusu ufugaji wa kisasa kwa lengo la kuleta tija katika sekta hiyo.

Akizungumza, leo Agosti 4, 2024 mkoani Dodoma alipotembelea kwenye Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa mkoani Dodoma katika mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Senyamule amesema wataalamu wahakikishe teknolojia hii inawafikia wadau wote wa mifugo na uvuvi, ususani maeneo ya vijijini.



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, (wa kwanza kulia), akielezewa na Ofisa maendeleo ya jamii wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Beatrice Mwijage (wa kwanza kushoto), juu ya Mpango wa unywaji Maziwa Shuleni, mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ni  katika Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma, Agosti 4, 2024, Dodoma.

"Wataalamu wachukue hatua ya kwenda kwenye makundi ya wafugaji ili kwenda kuwaelimisha kuhusu teknolojia mpya ya ufugaji na kuhakikisha inawafikia," amesema Senyamule

Aidha, amesema serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, imefanya mapinduzi makubwa  katika sekta ya Mifugo na Uvuvi kwani ameshuhudia teknolojia mbalimbali na nzuri katika mabanda ya Mifugo na Uvuvi.

Senyamule amesema hata sekta binafsi pia wamepokea mabadiliko hayo ya kiteknolojia, hususani upande wa vijana wa Jenga Kesho iliyo Bora (BBT) ambao wanatumia teknolojia hizi kama ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.

Vilevile  Senyamule ametoa wito kwa wadau wote wa Mifugo na Uvuvi  kutumia fursa hii ya maonesho haya ya nanenane ili kuweza kujifunza na kupata ufahamu juu ya teknolojia hii ya mifugo na uvuvi.


Comments

Popular posts from this blog

CHODAWU YAITAKA SERIKALI KURIDHIA MKATABA NAMBA 189 WA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI

NGOs ZAPEWA MWONGOZO WA KULIPA KODI NA TRA

TMDA YATOA MSAADA WA DAWA NA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SH 24 MILIONI