CHODAWU YAITAKA SERIKALI KURIDHIA MKATABA NAMBA 189 WA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI
Muhtasari: Wafanyakazi wa majumbani wameitaka serikali kuridhia mkataba namba 189 wa Shirika la kazi Duniani (ILO) ili kada hiyo iweze kutambulika kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine nchini. Na Mwandishi Wetu, Dodoma WAFANYAKAZI wa majumbani wameiomba serikali kuridhia mkataba namba 189 wa Shirika la kazi Duniani (ILO) kuhusu kazi za staha kwa wafanyakazi wa majumbani ili waweze kupata haki zao kama wafanyakazi wengine ikiwemo likizo, kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii na kulipwa kima cha chini cha mshahara. Kauli hiyo imetolewa leo jumanne na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Light for Domestic Workers (LDW) ambayo inajishughulisha na kutoa elimu kuhusu wafanyakazi wa majumbani kujua haki na majukumu yao, Beatrice Johnson wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa chama cha wafanyakazi wa mahotelini na majumbani (Chodawu) Jijini Dodoma. Beatrice amesema wafanyakazi wa majumbani wanapitia changamoto nyingi kwenye maeneo yao ya kazi kwa kuwa hakuna sheria inayowalinda kwan...


Comments
Post a Comment