WAISLAM WATAKIWA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

 Muhtasari: Waumini wa dini ya kiislamu wametakiwa kujitokeza kwa wiingi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ili waweze kuhoji au kupongeza yale yanayoendelea nchini.

Na Mwandishi wetu, Dodoma.

Dodoma. Waumini wa dini ya kiislamu nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kulingana na ratiba itakayotolewa na serikali.

Kauli hiyo imetolewa leo jumatatu Juni 17, 2024 na mwakilishi wa mufti wa Tanzania, Shekhe Swedi Twaibu kwenye ibada ya swala ya Eid El Adha iliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Shekhe Twaibu amesema ni jukumu la waumini wa dini hiyo kushiriki kila jambo ambalo kinaendelea nchini ili wawe nafasi ya kuhoji au kupongeza yale yanayoendelea nchini.

"Mufti wa Tanzania (Shekhe Aboubakar Zubeir) amenituma kwenu niwaambie kuwa mshiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa msiliache jambo hili liwapite mjitokeze kwa wingi kuwachagua viongozi watakaowaongoza kwa misingi ya haki," amesema Shekhe Twaibu.



Pia amewataka kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo ili waweze kuchagua na kuchaguliwa kwani ni haki yao ya msingi  endapo wana sifa zitakazotakiwa.

Mbali na hilo amewataka waumini hao kusherehekea kwa amani na utulivu sikukuu hii na kujiepusha na mambo mabayavyatakayowaletea matatizo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya sherehe za Idd Dodoma Mjini Shekhe Ismail Daudi amewataka waumini hao kuzingatia ujumbe ulitolewa na Mufti wa Tanzania kupitia mwakilishi wake kwani ni jukumu lao kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii na kiserikali.



Amesema suala la  kudumisha amani kwenye siku kuu hii ni la muhimu kwani wengi huwa wanazitumia vibaya kwa kulewa na kuendesha kwa fujo hivyo kuhatarisha maisha yao na ya watu wengine.

Akizungumza baada ya swala hiyo baadhi ya waumini wamesema wataitumia sikukuu hii  kukaa na familia zao kwa ajili ya kula na kunywa na watajiepuaha na matendo yote mabaya yaliyokatazwa na viongozi wa dini.

Mwisho....

Comments

Popular posts from this blog

CHODAWU YAITAKA SERIKALI KURIDHIA MKATABA NAMBA 189 WA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI

NGOs ZAPEWA MWONGOZO WA KULIPA KODI NA TRA

TMDA YATOA MSAADA WA DAWA NA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SH 24 MILIONI